# Maelezo ya jumla Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu. # Ni nani aliyezitengeneza mifereji Yahweh anatumia swali hili kutia mkazo kwamba yeye ndiye hufanya mambo haya yote. # gharika ya mvua "mbubujiko wa nguvy wa mvua" # njia "barabara'' au "sehemu za kupita" # milipuko ya radi "sauti ya radi." Hii ni sauti kuu ya radi ambayo hutoka katika mawimbi ya hewa. # kuifanya mvua inyeshe Yahweh hutengeneza mifereji ya chemichemi ya maji ili kwamba aweze kutuma maji juu ya nchi sehemu ambazo hakuna watu. # hakuna mtu aishiye ndani yake "sehemu isiyo na watu" # ili kutimiza mahitaji "ili kwamba mvua iweze kukidhi mahitaji" # mikoa iliyo kame na yenye ukiwa "sehemu ambazo hazina mimea au wanyama au watu" # majani mororo majani ambayo kwanza yameanza kukua na bado machanga na laini # kuyastawisha "kuanza kukua"