# Maelezo ya jumla Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu. # Wewe ulikuwa wapi... misingi Yahweh anaumia swali hili il kutia mkazo kwamba Ayubu hakuwepo wakati Mungu alipoumba dunia, hivyo Ayubu haelewi jinsi Mungu alivyoiumba dunia. # ilipoitandaza misingi ya dunia "Nilifanya misingi ya dunia" Yahweh anaelezea jinsi alivyoiumba dunia kana kwamba alikuwa akijenga jengo. # Niambie "Niambie jibu" # kama unao ufahamu zaidi "unadhani unajua sana" # ni nani aliyeamuru vipimo vyake Yahweh anatumia swali hili kutia mkazo kwamba ni yeye anayeamua namna ukubwa wa dunia unavyopaswa kuwa, hivyo ni yeye pekee anayejua jinsi alivyoifanya. # alivinyosha vipimo juu yake "aliipima dunia kwa kamba" # kipimo kamba ambayo watu waliitumia ili kuhakiki kuwa wanajenga jengo kwa kipimo halisi na kwa muundo sahihi.