# Maelezo ya jumla Elihu anaendelea kuzungumza # Na wakati akaapo kimya, nani aweza kumhukumu kuwa mkosaji? Elihu anatumia swali kwa ajili ya kumfundisha Ayubu. "Hakuna anayeweza kumkosoa Mungu kama akiamua kukaa kimya" # Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumjua? Elihu anatumia swali jingine kwa sababu ile ile. "Hakuna hata mmoja anayeweza kwenda na kumwona kama akiamua kujificha mwenyewe." # asiwepo mtu wa kuwanasa watu. Hii inawalinganisha watu watawaua na muwindaji ambaye hunasa nyara zake.