# Maelezo ya jumla Elihu anaendelea kuzungumza # Mungu ambaye humwambia mfalme, ' Wewe ni mbaya; au huwaambia wenye kuheshimiwa, 'Ninyi ni waovu'? Hii inaendeleza swali kutoka katika mstari uliotangulia. # mbaya "mwovu" au "asiyestahili" # , kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake Mahali hapa neno "mkono" linamaanisha nguvu. # wakati wa usiku watu watatikiswa na watapita "wakati wa usiku" ni wakati wa mwisho wa siku na mwanzo wa siku nyingine. # watu wenye nguvu watatwaliwa mbali,lakini si kwa mikono ya wanadamu. "Ni Mungu wala si wanadamu anayewafanya watu wa muhimu wafe.