# Maelezo ya jumla Elihu anaendelea kuzungumza # usikilize hotuba yangu; sikiliza maneno yangu yote Virai hivi viwili vinamaanisha kitu kimoja. Elihu anatia mkazo kwamba Ayubu lazima asikilize kwa makini. # nimeufumbua mdomo wangu; ulimi wangu umesema maneno ndani ya mdomo wangu Kauli hizi zinamaanisha kitu kimoja. Elihu anatiza mkazo kwamba sasa ana utayari wa kuzungumza. # Maneno yangu yatasema uadilifu wa moyo wangu "Nitazungumza kwa ukamilifu wa uadilifu" # yatasema kwa unyofu yale ambayo mdomo wangu unayajua. "Nitakwambia kwa uaminifu mambo ninayoyajua"