# Maelezo ya jumla Elihu anaendelea kuzungumza kwa kutumia mtindo wa usambamba # nimejawa na maneno "nina mengi sana ya kusema" # roho ndani yangu inanisukuma "lazima niseme sasa" # kifua changu ni kama divai yenye chachu ambayo haina tundu; kama viriba vipya, kiko tayari kupasuka. Wakati divai inapochacha, gesi hujikusanya katika chombo. Kama gesi hiyo yaitaondolewa, chombo kitapasuka . Elihu anamaanisha kwamba anayo mengi ya kusema na kama hatayasema anajisikia kama atapasuka.