# Maelezo ya jumla Ayubu anaendelea kuzungumza # kama nime... Katika 31:5-40 Ayubu anafafanua hali mbalimbali ambazo angesitahili kupata hukumu ya Mungu. Lakini anajua kuwa si ya kweli na yeye hana hatia. # nimetembea katika udanganyifu, kama mguu wangu umeharakisha katika uongo "kufanya kitu cha uongo au kumdanganya mtu kwa makusudi" # na nipimwe katika vipimo vilivyo sawa Watu hutumia mizani ili kupima vitu na kutambua uthamani wake. "Mungu na anihukumu kwa uadilifu"