# Maelezoa ya jumla katika mistari ya 18-28 Ayubu anasimulia mambo ambayo alifanya kabla mambo mabaya hajatokea kwake. # nilivunja taya za ... nilimng'oa mwathirika " niliwafanya dhalimu waache kuwatesa watu, kam mtu anayevunja taya la mnyama mwitu na kuokoa mhanga kutoka katika meno yake" # nitakufa katika kiota changu " nitakufa kwenye nyumba yangu pamoja na familia yangu" au "nitakufa katika usalama wa nyumbani kwangu" # nitazidisha siku zangu kama mchanga "nitaishi maisha marefu" au "nitaishi miaka mingi " # Mizizi yangu ... matawi yangu Ayubu anaongea juu ya nguvu zake, anasema yeye ni kama mti imara uliomwagiliwa vizuri.