# Nilivaa haki, nayo ikanifunika watu wa wakati ule waliongelea haki kama vazi. KTN: "Nilitenda haki, nayo ikawa kama vazi la kujisitiri juu yangu" # uadilifu wangu ulikuwa kama joho na kilemba watu wa wakati ule waliongelea uadilifu kama vazi. KTN: "Nilitenda kwa adili, na ilikuwa kama joho na kilemba juu yangu" # kilemba vazi refu ambalo wanaume hufunga kuzunguka vichwa vyao, huvaa kama kofia. # nilikuwa macho kwa watu vipofu Hii inamaanisha kuwasaidia watu vipofu. KTN: "nilikuwa kama macho kwa ajili ya watu vipofu" au "niliwaongoza watu vipofu" # nilikuwa miguu kwa watu viwete "nilikuwa kama miguu kwa watu viwete" au "niliwasaidia watu viwete" # nilikuwa baba kwa watu wahitaji hapa neno baba linawakilisha kutoa kwa ajili ya watu. KTN: "Nilitoa kwa ajili ya watu wahitaji kama baba anavyotoa kwa ajili ya watoto wake"