# Basi, hekima hutoka wapi? Mahali pa ufahamu ni wapi? Ayubu anatumia maswali haya kudokeza jinsi gani watu hupata ufahamu na hekima> KTN: " Nitawaambia hekima hutoka wapi na mahali ufahamu ulipo" au "nitawaambia jinsi ya kuwa na busara na namna ya kujifunza vitu vya ufahamu" # Basi hekima hutoka wapi hekima inaongelewa kana kwamba ipo mahali fulani na huwajia watu. hii inamaanisha watu kujipatia busara. KTN: "Basi watu hupata wapi hekima" au "basi namna gani watu hupata busara" # Mahali pa ufahamu ni wapi Ufahamu umeongelewa kama kitu ambacho kipo hali. KTN: "Watu hupata wapi ufahamu" au "namna gani ya watu hufahamu vitu" # hekima imefichwa kutoka kwenye macho ya viumbe hai vyote Viumbe hai haviwezi kuiona hekima. KTN: "Hakuna kiumbe hai chenye kuweza kuiona hekima" # na imefichwa kutoka kwa ndege wa mbinguni "hata ndege ambao huruka katika anga hawawezi kuona hekima" # uharibifu na mauti husema hapa "uharibifu" na "mauti" ni tamathali kwa sehemu ambapo watu huelekea wakati wanapofariki.