# Maelezo ya Jumla kwenye 28:12-28, hekima na maarifa vimesemwa kama vitu ambavyo vipo mahali fulani na watu wanataka wavipate. kutafuta hekima na maarifa inawakilisha kuwa na busara na kujifunza kufahamu vitu kwa uzuri. # Je hekima itapatikana wapi? Je ni sehemu gani yenye maarifa? Maswali haya yanamaana moja na yametumika kuonesha kuwa ni vigumu kupata hekima na maarifa. # Je hekima itapatikana wapi? Je ni sehemu gani yenye maarifa Kuwa mwenye hekima na maarifa inazungumziwa kana kwamba ni kutafuta hekima ana maarifa: KTN: "Jinsi gani watu huwa na hekima? Jinsi gani watu hujifunza kufahamu vitu kwa uzuri?" # Binadamu hajui thamani yake Hapa inaweza kumaanisha kuwa:- 1) "Watu hawajui uzuri wake" au 2) "Watu hawajui mahali ilipo" # wala haipatikani katika nchi ya walio hai nchi ya walio hai inamaana ya ulimwengu huu ambapo watu wanaishi. KTN: "na hakuna mtu anayeweza kupata hekima katika ulimwengu huu " # Maji yenye kina... yanasema, 'haiapo ndani kwangu' bahari inasema, ' haipo kwangu' vilindi vya maji na na bahari vinasimama kama watu wanaoweza kuongea. KTN: "Hekima haipo ndani ya vilindi vya maji chini ya ardhi, wala katika bahari"