# wale ambao husalia Hii inahusu watoto wa mtu mwovu ambao huendelea baada ya baba zao kufariki. KTN: "Wale ambao huendelea kuishi baada ya baba zao waovu kufariki" # watazikwa kwa tauni "watakufa kwa tauni" # wajane wao... yao maneno "wao... yao" yanahusu wale watakaosalia, ambao ni watoto wa mtu mwovu # hurundika fedha kama mavumbi "hurundika "maana yake hukusanya sana. Ayubu anasema kuwa ilikuwa rahisi kwa mtu huyu kujipatia fedha kama vile mavumbi. # hurundika mavazi kama udongo "hurundika "maana yake hukusanya sana. Ayubu anasema kuwa ilikuwa rahisi kwa mtu huyu kujipatia mavazi kama vile kuzoa udongo.