# jinsi gani ulimsaidia yule ...mkono ambao hauna nguvu! Ayubu anamshutumu Bildadi. Neno "yule" linamrejea yeye mwenyewe (Ayubu). KTN: "Mimi sina uwezo wal nguvu, lakini unajifanya kama umenisaidia- ukweli ni kwamba hujanisaidia kabisa!" # mkono ambao hauna nguvu Ayubu anajielezea mwenyewe kuwa..."mimi, ni kama mkono ambao hauna nguvu au "yule ambaye ni dhaifu kabisa" # Jinsi gani umemshauri yule asiyekuwa na hekima na kumtangazia maarifa ya kweli! Ayubu anasema kwamba Bildadi hajatoa ushauri mzuri wala maarifa kwake. KTN: " Umetenda kana kwamba hauna maarifa kwa njisi ulivyonishauri" # kumtangazia maarifa ya kweli "kumpa ushauri mzuri" # Kwa msaada wa nani umeongea maneno haya? je ilikuwa roho ya nani... yako? katika maswali haya Ayubu anaendelea kumdhihaki Bildadi. KTN: "lazima ulipata msaada kuongea maneno haya. Yamkini roho fulani ilikusaidia kuyaongea maneno haya"