# Bildadi Mshuhi hili ni jina la mtu kama ilivyo katika 2:11 # Milki na hofu vipo pamoja naye "naye" inarejea kwa Mungu. majina ya dhahania "milki" na "hofu" yanaweza kutajwa kama vitenzi. KTN: "Mungu ni mtawala wa yote, na watu wanapaswa kumhofu yeye peke yake" # katika sehemu zake za juu mbinguni "katika mbingu" au "kwenye mbingu juu" # Je kuna ukomo wa idadi ya majeshi yake? Bildadi anatumia swali hili kueleza jinsi Mungu alivyo mkuu. KTN: "Hakuna ukomo wa idadi ya malaika katika jeshi lake" au Adui zake ni wakubwa sana kwamba hakuna awezaye kuwahesabu" # je ni juu ya nani mwanga wake haumuliki? Bildadi anatumia swali hili kueleza kwamba Mungu hutoa mwanga kwa kila mtu. KTN: "Wala hapana mtu ambaye mwanga wake haumuliki" au "Mungu hufanya mwanga wake kung'aa juu ya kila mmoja"