# Sentensi Unganishi Ayubu anaendelea kuongea # Tumbo hii inarejea kwa mama. KTN: "mama" # minyoo itamla na kuona utamu hii inamaana kuwa atakufa na minyoo itaula mwili wake. KTN: minyoo itafurahia kula mzoga wake" au "atakufa na mwili wake utaliwa na minyoo" # hatakumbukwa tena " hakuna mtu atakayemkumbuka tena" # utavunjwa kama mti " Mungu atawaharibu waovu kama mti" # mwovu huteketeza sitiari hii inasisitiza jinsi mtu mwovu asivyofaa. KTN: "Kama mnyama mwitu anavyoua mawindo yake, ndivyo mtu mwovu huleta maumivu" # wanawake tasa ambao hawakuzaa watoto watu wa wakati ule waliamini kuwa mtu ambaye hakuzaa watoto alikuwa amelaaniwa na Mungu. Hii inawakilisha wanawake wenye bahati mbaya kabisa.