# Sentensi Unganishi Ayubu anaendelea kuongea # kama povu juu ya uso wa maji povu hudumu kwa muda mchache. Hii inasisitiza kuwa Mungu atasababisha waovu wapotee upesi. # sehemu ya ardhi yao imelaaniwa KTN: "Mungu hulaani sehemu ya ardhi ambayo wanamiliki" # Kama ukame na joto huyeyusha...wale ambao wamefanya dhambi Ayubu anasema kwamba wenye dhambi watapotelea kuzimu kwa njia ile ile kama vile theluji inavyoyeyuka na kupotea inapokuwa joto. # ukame na joto haya maneno mawili yanaelezea hali ya hewa inayofanana.