# Sentensi Unganishi Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake. # Ni nani ataishutumu njia ya mtu mwovu kwenye uso wake? Ayubu anatumia swali hili kupinga dhana ya kuwa waovu mara zote hupatwa na hukumu. KTN: ' Hakuna anayemshutumu mtu mwovu kwenye uso wake" # kwenye uso wake Hapa inamaana kuwa hakuna mtu atakaye kwenda moja kwa moja kwake na kumshutumu. # Ni nani atamlipiza kwa yale aliyotenda? Ayubu anatumia swali hili kupinga imani ya rafiki zake kuwa waovu mara zote hupatwa na hukumu. KTN: ' Hakuna mtu anayemlipiza mwovu kwa mambo mabaya aliyotenda" # atazikwa KTN: " Watu watambeba" # Madonge ya bondeni yatakuwa matamu kwake Maana yake ni kwamba mtu mwovu atakuwa na kifo chema na maziko mema baada ya kutimiza maisha yake. KTN: "atafurahia kufukiwa kwa uchafu wa bondeni" au " atafurahia kuzikwa katika uchafu wa bonde" # watu wote watamfuata, kutakuwa na watu wengi mbele yake Ayubu anaweka makazo kuwa kundi kubwa la watu watakuwepo katika harakati za mazishi yake kutoa heshima. KTN: "idadi kubwa ya watu watakwenda kwenye eneo la makaburi; baadhi wakiwa mbele na wengine nyuma"