# Sentensi Unganishi Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake. # Mtu yeyote anaweza kumfundisha Mungu maarifa ikiwa yeye huwahukumu hata wale walio wakuu? Ayubu anauliza swali kusisitiza kwamba Mungu anajua kila kitu. KTN: "Ni wazi, hakuna mtu anayeweza kumfundisha Mungu chochote kwani yeye huwahukumu hata wale walioko mbinguni." # walio wakuu inaweza kumaanisha kuwa 1) "wale walioko mbinguni" au 2) "watu mashuhuri" # mtu mmoja hufa katika nguvu zake kamili. Ayubu anamlinganisha mtu huyu afaye katika afya na amani na mtu afaye katika hudhuni na maumivu. KTN: "Kama kuma watu wawili, mmoja anaweza kufa katika nguvu zake kamili" # mwili wake umejaa maziwa hii inamaana kwamba mtu yupo katika afya njema. # mwili wake umejaa maziwa... uboho wa mifupa yake umarainishwa na katika afya nzuri. hii inamaana kwamba mtu yupo katika afya njema. # mwili wake umejaa maziwa Neno "maziwa" linamaana ya "mnene" KTN: "mwili wake umejaa mafuta" # uboho wa mifupa yake umarainishwa na katika afya nzuri. hii ni nahau ikimaanisha kuwa mwili wake una ujana na afya njema.