# Habari za Jumla: Ayubu anaendelea kuzungumza kwa Mungu. # Ninyi daima humshinda yeye, Neno " yeye" linamaanisha kila mtu" Ninyi daima mnamshinda mwanadamu" au " Ninyi daima mnawashinda watu" # yeye hupita mbali; Kupita mbali kunawakilisha kufa. " yeye hufa" # Ninyi mnabadilisha uso wake Maana zaweza kuwa hizi: Maumivu kabla ya kufa humfanya uso wake kuwa angavu, au wakati mtu anapokufa, Mungu huufanya uso wa mtu kuwa tofauti. # kumtuma yeye mbali kufa Sentensi hii inawakilisha kumsababishia yeye kufa. # na kama wakishushwa chini, Kushushwa chini ni kuaibishwa. " kama wao wameaibishwa" au " ikiwa watu wakiwaaibisha wao"