# Habari za Jumla: Sura hii ni mwendelezo wa hotuba ya Ayubu, iliyoanza 12:1. Ayubu anazungumza kwa Mungu. # Mwanadamu, ambaye amezaliwa na mwanamke, Sentensi hii ina maanisha watu wote,wanaume na wanawake wote wamezaliwa katika ulimwengu huu. # huishi siku chache tu hapa imetumika lugha ya kukuza jambo ili kutoa msisitizo kwamba watu huishi muda mfupi tu. " hushi muda mfupi sana" # amejaa mahangaiko. Kujaaa "mahangaiko" inaonyesha kupata mateso mengi. "yeye ana mahangaiko mengi" au " anateseka sana" # Yeye huchanua kutoka katika ardhi kama ua na kukatwa chini; Kama maisha ya ua, maisha ya mtu ni mafupi na ni rahisi kuuawa. # yeye hukimbia kama kivuli na hawezi kudumu. Maisha mafupi ya mwanadamu yamelinganishwa na kivuli ambacho hutoweka haraka. # Je, wewe unatazama chochote katika hivi? Ayubu ana maanisha kuwa yeye hahitaji Mungu amsikilize sana." Wewe hautazami chochote haya" au " Wewe haunisikilizi sana mimi " # tazama katika hivi Kumtazama mtu kunawakilisha kuwa makini kumsikiliza ili kumhukumu yeye. "Kuwa tayari kusikiliza" au " tazama makosa ndani yake" # Mnanileta mimi hukumuni pamoja nanyi? Ayubu anatumia swali hili kuonyesha kushangaa kwake kuwa Mungu anamhukumu yeye ingawa Ayubu si wa thamani kama ua."Lakini wewe wanihukumu mimi"