# Hakuna shaka "Hakika" # ninyi wanadamu "ninyi ni watu muhimu mnafahamu kila kitu" # Hakuna shaka ninyi wanadamu; Hekima mtakufa nayo Ayubu anawadhihaki jinsi gani wanavyotenda na kuonyesha jinsi walivyo wenye kudhihaki. "Hakika ninyi ni watu muhimu kwamba hekima haiwezi kuwepo bila ninyi" au " Ninyi nyote mnatenda kama ninyi ni watu wenye hekima peke yenu, na kwamba wakati mtakapokufa hekima itapotea" # ninyi Huu ni wingi hapa na katika sentensi mbili zifuatazo. # Ni dhahiri, ni nani asiyefahamu vitu hivyo kama hivi? Ayubu anatumia swali hili kuelezea ukweli ambao unapaswa kuwa wazi kwa wasikilizaji wake. Sentensi hii inaweza kuelezwa kwa jinsi hii: Ni dhahiri hakuna awaye yote ambaye hafahamu vitu kama hivi" au "kila mtu anafahamu vitu hivi"