# Je si siku zangu pekee ni chache? Hapa "siku zangu" zinahusiana na urefu wa maisha ya Ayubu. Swali hili linataraji jibu halisi, kusisitiza kwamba Ayubu anatazamia tu kuishi siku chache zaidi. Inaweza kutafsiriwa kama taarifa. "Mimi nina siku chache tu za kuishi zilizobaki."au "Maisha yangu hivi karibuni yatafikia mwisho." # nchi Hapa sehemu ambayo roho za watu waliokufa huenda inazungumziwa kana kwamba ilikuwa nchi. "sehemu" # kwenye nchi ya giza na kivuli cha mauti Kifungu "kivuli cha mauti" inaongeza wazo la "giza." Vifungu vyote vinaelezea wapi roho za watu waliokufa huenda. # kivuli cha mauti Fasiri kifungu hiki kama katika 3:4 # giza kama usiku wa manane Giza la sehemu ambapo roho za watu walio kufa huenda inalinganishwa na giza la usiku wa manane. # bila mpangilio Hiki kifungu cha kukanusha kinaweza kuelezewa katika hali halisi. "wasiwasi mwingi" au "sehemu ambayo wote wamechanganyikiwa" # ambayo nuru yake ni kama usiku wa manane Mwanga wa sehemu ambayo roho za watu waliokufa huenda inalinganishwa na usiku wa manane. "ambapo hakuna nuru"