# ulinitoa kwenye tumbo la uzazi Hapa kutolewa nje la tumbo la uzazi kunahusiana na kuzaliwa duniani. "kunitoa mimi nje la tumbo la uzazi la mama yangu" au " kunileta mimi duniani" # ningekata roho Kukata roho kwa mtu kunahusiana na kufa. "fariki" # na ili jicho lolote lisinione Ayubu anatumia "jicho" hapa akirejea watu wote. Anatamani yeye angelikufa wakati wa kuzaliwa, kabla hajaonekana na yeyote. "kabla mtu yeyote hajaniona mimi" au "kabla ya kuzaliwa kwangu" # kuwepo "kuishi" # ningelikuwa nimechukuliwa "Mwili wangu ungelikuwa umechukuliwa"