# Nimechoka na maisha yangu "mimi nimechoka kuishi" # Nitanena wazi manung'uniko yangu Jina la kufikirika "usemi" na "lalamiko" yanaweza kutafasiriwa kama vitenzi "eleza" na "nung'unika." "Mimi nitaeleza wazi kile ninachonung'unikia" au "Mimi nitahoji wazi" # nitasema kwa uchungu wa roho yangu Namna gani Ayubu anavyojisikia inalinganishwa na ladha chungu. Jina la kufikirika "chungu sana" inaweza kutafasiriwa kama kielezi "chungu." "Utu wangu wa ndani utaongea kwa uchungu" au "Kwa uchungu nitasema sana" # ni vizuri kwako wewe kunionea mimi, kudharau kazi ya mikono yako wakati unafurahia juu ya mipango ya waovu? Swali hili linahitaji jibu la "hapana" na inaweza kubadilishwa na kuwa habari. "Si vyema kwamba unaweza kunikandamiza mimi, kwamba unaweza kudharau kazi ya mikono yako, wakati ukifurahia juu ya mipango ya waovu." # kazi ya mikono yako Hapa mikono inawakilisha uwezo wa kuumba wa Mungu. "kile ulicho kiumba" # unafurahia juu ya mipango ya waovu Hapa usemi "ridhia" ni mfano wa kibali cha Mungu."kubali mipango ya waovu"