# Habari za Jumla: Mwandishi anaendelea kutumia ulinganishaji katika mistari miwili ya kwanza, kuwasilisha wazo moja akitumia taarifa mbili tofauti kuelezea maumivu makali sana ya Ayubu. # kitanda changu kitanifariji, na malazi yangu yatatuliza manung'uniko yangu Hapa "kitanda" na "malazi" ni mifano wa "kulala." Kwa kulala chini, Ayubu alitarajia faraja. Mfano pia una sifa za kibinadamu; wana uwezo wa kumriwadha na kumfariji mtu. # wewe unanitisha mimi "wewe" inamaanisha Mungu ambaye Ayubu anamlalamikia. # kunyonga kuua mtu kwa kumkaba koo lake na kuzuia asipumue. # hii mifupa yangu Hapa Ayubu anatumia neno "mifupa" kumaanisha mwili wake. "Huu mwili wangu"