# Habari za Jumla: Katika mistari hii, Elifazi anaendeleza hotuba toka 4: 1. Mwandishi anaenedelea kutumia ulinganishaji katika kila mstari, kuwasilisha wazo moja akitumia maelezo mawili tofauti kusisitiza kwamba Ayubu lazima akiri hali yake kwa Mungu ambaye hutenda mambo ya kustajabisha. # makuu na mambo yasiyochunguzika, mambo ya ajabu yasiyo na hesabu "Mambo makuu ambayo hayawezi fahamika, maajabu ambayo hayahesabiki" # mambo yasiyochunguzika Hii inamaanisha mambo ambayo wanadamu hawezi kuyaelewa. # makuu na mambo yasiyochunguzika Hapa mwandishi anatumia maneno mawili yanayojitegemea na kuunganishwa kwa "na" kusisitiza ukuu wa matendo ya Mungu. "mambo makuu sana yenye kuhitaji maarifa mengi" # mambo ya ajabu "mambo ya kustajabisha" au "maajabu"