# Habari za Jumla: Mistari hii inaendeleza matumizi ya awali ya ulinganishaji, hapa inasisitiza katika njia tofauti wazo kwamba watu hufa ghafla pasipo kupata hekima na wala usumbufu kutoka kwa wengine. # Kati ya asubuhi na jioni wameangamizwa Hii inamaanisha wazo la kitu fulani kinachotokea upesi. # wameangamizwa Hii pia inaweza kuwekwa katika umbo hai. "wamekufa" # Je kamba za hema yao hazikung'olewa kati yao? Hii inaweza kuwekwa katika umbo hai. "Si adui zao waliong'oa kamba za hema zao kutoka miongoni mwao?" # kamba za hema yao Hapa kamba za hema zinawakilisha hema. Wakati mwingine nyumba ya mtu na familia zinafananishwa kama hema yake, ambayo inaweza pia kuwakilisha mali zake zote.