# Habari za Jumla: Mwandishi anatumia ulinganishaji katika mistari hii, anawasilisha wazo moja akitumia maelezo tofauti kutilia mkazo uharibifu wa Mungu kwa watu waovu. # Kuunguruma kwa simba, sauti ya simba mkali, meno ya simba wadogo - yamevunjika. Hapa muungurumo wa simba, sauti yake, na meno yake yamevunjika vinatumika kama mfano wa kuangamizwa kwa waovu. # yamevunjika Hii inaweza kuwekwa katika umbo halisi. "kitu fulani kimeyavunja" # Simba mzee huangamia kwa kukosa wahanga; watoto wa simba jike wametawanyiko kila mahali Elifazi anatumia picha ya simba mzee anayekufa kwa njaa na familia yake imetawanyika kama sitiari ya kuangamizwa kwa waovu # wametawanyika "kitu fulani kimetawanya watoto wa simba"