# Habari za Jumla: Ayubu anabadilisha mazungumzo yake kutoka kufa mpaka uzima baada ya kifo. # Huko waovu huacha kusumbua; huko waliochoka hupumzika. Ayubu anatumia usambamba kusisitiza kuwa wanyonge watapata pumziko kutoka kwa wale walio wasababishia magumu. # Huko waovu huacha kusumbua Ayubu anaongea kuhusu sehemu ambayo watu huenda baada ya wao kuacha kuishi. "Katika sehemu hiyo, watu waovu huacha kusumbua" # sauti ya msimamizi wa watumwa Hapa "sauti" ni mfano wa nguvu ambayo msimamizi wa watumwa anakuwa nayo juu ya watumwa. "Hawako tena chini ya udhibiti wa watumwa" # wadogo na watu maarufu Hii ni tamathali ya usemi ambayo humaanisha "watu wote, watu masikini na watu matajiri." # mtumishi yuko huru kwa bwana wake huko. Mtumishi hana wajibu wa kumtumikia bwana wake.