# Habari za Jumla: Ayubu anaendelea na fikira zake kuhusu kufa kabla ya kuzaliwa. # Au Ningelikuwa nimelala pamoja ... wasio uona mwanga kabisa. Hii inaelezea kitu ambacho kingetokea lakini hakikuweza kutokea. # Au Ningelikuwa nimelala pamoja na wakuu "Ningelikuwa nimepumzika na wakuu." Katika kifungu hiki, neno "lala" na "kupumzika" ni njia ya heshima kusema "haishi tena." # wenye dhahabu, waliozijaza nyumba zao fedha Ayubu anatumia ulinganishaji kusisitiza kile anachosema. # Au pengine ningekuwa sijazaliwa, kama watoto wachanga wasio uona mwanga kabisa. Ayubu anatumia ulinganishaji kusisitiza anachosema. # ningekuwa sijazaliwa "Ningelikuwa nimekufa tumboni mwa mama yangu" # kama watoto wachanga wasio uona mwanga kabisa "kama watoto wachanga ambao hawangelizaliwa" # watoto wachanga "watoto" au "watoto wadogo sana"