# Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi Elifazi, Bildadi, na Sofari ni majina ya wanaume. Temani ulikuwa mji katika Edomu. Washuhi ni uzao wa Ibrahimu na Ketura (tazama Mwanzo 25: 1). Naamathi ulikuwa mji katika Kanaani. # Wakatenga muda "walikubaliana juu ya wakati" # kuomboleza naye na kumfariji. Hapa neno "omboleza" na "fariji" yana maana sawa. Rafikize wanajaribu kumfariji Ayubu na kuomboleza naye. "kuhuzunika na Ayubu ili kusaidia kupoza mateso yake."