# Je hata sasa wewe unashikamana na utimilifu wako? Hili swali la kejeli kwa kweli linatengeneza taarifa. Tafasiri kama katika 1: 6. "Angalia mtumishi wangu Ayubu." # Umkufuru Mungu "Kumkataa Mungu" # unaongea kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu Ayubu akasema unaongea kama mwanamke mpumbavu. "Unaongea kana kwamba wewe ni mwanamke mpumbavu." # Je sisi tupate mema toka kwa Mungu na tusipate mabaya? Swali hili la kejeli kwa kweli linawasilisha taarifa. "Bila shaka lazima tungelipata mabaya kutoka kwa Mungu pamoja na mazuri." # tupate mema "kunufaika na mambo yote mazuri" # mema Hili linawakilisha mambo yote mazuri ambayo Mungu hutupa. # tupate mabaya "teseka na mateso yote mabaya bila kulalamika" # mabaya Hili linawakilisha mambo yote mabaya ambayo Mungu hufanya au huruhusu ili sisi tupate maarifa. # tenda dhambi kwa midomo yake. Hapa "midomo" inawakilisha tendo la kuongea. "dhambi kusema kwa kushindana na Mungu"