# Taarifa za jumla: Huu ndio mwisho wa Injili ya Yohana. Hivyo mwandishi ambaye ni Yohona anatoa salamu za mwisho na kusema kidogo kuhusiana na yeye mwenyewe. # mwanafunzi mwanafunzi wa Yohana # ambaye hushuhudia kuhusu mambo yaleyale neno kushuhudia kama lilivyotumika hapa linamaanisha kuona kitu # sisi tunajua "sisi" hapa inamaanisha wale wanaomwamini Yesu # kama kila kitu kingeandikwa unaweza kutafsiri pia kwa kusema, "kama mtu angeandika kila kitu" # hata dunia pia isingeweza kutosha vitabu vyote Yesu alifanya miujiza mingi kuliko ambavyo watu wangeweza kuandika kwenye vitabu