# Amini, amini Tafsiri kama ulivyofanya katika Yoh. 1:49 # Mimi ni mlango wa kondoo "Mimi ni njia wanayoipitia kondoo kwenda zizini." Yesu anasema yeye ndiye anayeruhusu kuingia. Neno "kondoo" limetumika kumaanisha watu wa Mungu. # Wote waliokuja kabla yangu Hili linarejea kwa walimu wengine waliofundisha kabla ya Yesu. # wezi na wanyang'anyi Yesu anawaita "wezi na wanyang'anyi" kwa sababu mafiundisho yao yalikuwa ya uongo, na walikuwa wakkijaribu kuwaongoza watu wa Mungu wakati hawaujui ukweli.