# Sisi Neno sisi linawahusisha wote Yesu na wanafunzi wake aliokuwa akiongea nao. # Mchana...Usiku Yesu analinganisha wakati watu wanaweza kufanya kazi wakait wa mchana, wakati ambao kwa kawaida watu hutenda kazi, na wakati wa usiku watu hawawezi kufanya kazi ya Mungu. # Nuru ya Ulimwengu Yule ambaye aonyeshaye kile kilicho cha kweli kama vile nuru ionyeshacho kilicho halisi.