# maji yao "maji" inawakilisha vyanzo vyote vya maji hasa mito inayopita kwenye mji. # Mbweha Mbweha ni mbwa mwitu wanaopatikana Asia na Afrika. # Mbuni wataishi kwake "mbuni" ni ndege mkubwa wa Afrika anayekimbia haraka lakini hawezi kupaa. Neno "kwake" linamaanisha Babeli. # Kwa muda wote hatakuwa mwenyeji. Kizazi hadi kizazi hakitaishi kwake. Sentensi hizi zina maana inayofanana zikisisitiza kuwa Babeli haitakuwa na wenyeji kabisa. # Hataishi ndani yake "hakuna atakayeishi kwake" # hakuna atakayeishi huko; hakuna atakayekaa kwake Maneno haya yanamaana moja yakisisitiza kuwa Babeli haitakuwa na wenyeji kabisa.