# Adui atapaa kama tai na kutandaza mabawa yake Hii inalifananisha jeshi lenye nguvu litaivamia Moabu na kuiteka kama vile tai anaposhuka chini na kukamata mawindo. # Keriothi. Ni mji katika Moabu. # Keriothi imekamatwa na ngome zake zimetekwa "Adui wameikamata Keriothi na kuteka ngome zake" # siku ile moyo wa askari wa Moabu ... wanawake wenye uchungu Sentensi hii inaonesha kuwa hofu itawapata askari wa Moabu kama hofu ambayo wanawake huipata wanapokaribia kuzaa.