# upaa Hiki ni kitendo cha kunyoa nywele zote za kichwani au sehemu ya nywele kama ishara ya maombolezo makubwa yanayofanywa na wanaoabudu sanamu wa mataifa kama Filisti. # watu ... watanyamaziswa. "Watu ... watauawa." # Kwa muda gani mtajikata wenyewe kwa ajili ya kuomboleza Kujikata ngozi ilikuwa inafanywa na wanaoabudu sanamu walipokuwa wakiomboleza msibani. # upanga wa Bwana Hili ni jeshi ka kaskazini ambalo Bwana analitumia kuwaadhibu Wafilisti. # Itachukua muda gani mpaka mtakapokuwa kimya Wafilisti walitumia swali hili kuonesha namna ambavyo walichanganyikiwa kutokana na uharibifu uliosababishwa na adui zao. # wewe Hapa upanga wa Bwana unafananishwa na mtu. # ala Ni kifaa kinachotumika kulindia makali ya upanga. # Ukuwaje kimya, kwa kuwa bwana amekuamuru Hapa unazungumziwa upanga wa Bwana.