# Taarifa ya jumla: Yeremia anaendelea kunukuu maneno ya Bwana kwa taifa la Misri. # Huyu ni nani anayeinuka kama mto Nile "Misri anainuka kama mto Nile." Bwana anauliza hili swali ili kuwafanya wasikilizaji wawe makini na taifa la Misri. # Misri imeinuka kama mto Nile Jeshi la Misri linasababishwa na uharibifu unaosababishwa na mafuriko ya mto Nile. # Unasema Hapa nchi ya Misri inazungumza kama mtu azungumzapo. # "Nitakwenda juu; nitaifunika nchi. Nitaharibu mji na wakaao ndani yake." Hapa taifa la Misri linajisifu na kusema kuwa jeshi lake litaharibu dunia kama mafuriko. # kwenda juu, farasi. kukasirika, magari yenu. Bwana anaamuri farasi na magari kama vile anaamuru watu. maneno haya "farasi" na "magari" yamezungumziwa kama sehemu ya vita. # Kushi ... Puti ... Ludimu Haya ni majina ya biblia ya nchi za Ethiopia, Libya na Lydia. # kukunja pinde zao Hiki ni kitendo cha kuupindisha upinde wenye mshale.