# Kisha wao Neno "wao" linawaelezea wakuu. # Wakakiweka kitabu katika chumba cha Elishama "wakakiweka kitabu sehemu salama katika chumba cha Elishama" # Elishama karani "Elishama aliyekuwa mwandishi" # Maneno haya Maneno ya kwenye kitabu ambayo Yeremia alimsomea Baruku. # Yehudi Hili ni jina la mtu. # katika mwezi wa tisa Huu ni mwezi wa tisa kwa kalenda ya Kiebrania. Majira haya ni mwishoni mwa msimu wa kupanda na mwanzo wa kipindi cha baridi. # Na mkaa ulikuwa ukiwaka mbele yake "Na mkaa ulikuwa mbele yake ukiwa unawaka" # Makaa Ni sehemu ya moto ambayo mtu anaweza kuihamisha