# Ikatokea kwamba Maneno haya yanaonesha umuhimu wa tukio katika simulizi. # Wao waliposikia Neno "wao" linamaanisha wakuu. # Maneno haya yote maneno yote ambayo Baruku aliyasoma kwa nguvu toka kwenye kitabu. # Uliyaandikaje "uliyaandika kwa namna gani" # Aliyosomewa na Yeremia "Yeremia alipokuwa akizungumza, Baruku aliandika maneno yote ambayo Bwana aliyazungumza kwa Yeremia" # Kusema Yeremia alizungumza kwa nguvu ili Baruku aandike maneno yake. # kuyaandika na wino "alitumia wino kuandika" # wino Wino mweusi unaotumika kuandikia # Na Yeremia pia "Yeremia pia anatakiwa ajifiche." # Mko wapi Maneno haya yanawaelezea Baruku na Yeremia.