# Maelezo ya jumla: Mungu anaendelea kusema tangu mstari wa saba. # Jiwekee alama za bara bara ... Weka matangazo ... Iweke akili yako ... Rudi. Virai hivi vimeelekezwa kwa "bikra Israeli." # Iweke akili yako juu ya njia sahihi, njia unayopaswa kufuata. "Jitahidi sana kukumbuka jinsi ulivyokuja kipindi ulipokuwa umechukuliwa mateka." # Rudi, bikra Israeli! Mungu anamtaja Israeli aliyebadilika. # Utatanga tanga hadi lini, binti usiyemwaminifu? Mungu anauliza kuwa mpaka lini watu wake watamuasi."Msisite site kuanza kunitii mimi."