# Maelezo ya jumla: Yahwe anaendelea kuzungumza. # Kusanyiko lao litaanzishwa mbele yangu. "Nitawaanzisha kama kundi la watu mbele yangu." # Kiongozi wao atatoka miongoni mwao. Atatokeza kutoka kati yao. Sentensi hizi mbili zina maana moja. sentensi ya pili inaimarisha au kufafanua wazo lililo katika sentensi ya kwanza; "Kiongozi wao atachaguliwa kutoka kwa watu." # Ni nani atakayethubutu kunisogelea? Yahwe anatumia swali kuweka msisitizo kwamba hakuna mtu mwenye ujasiri wa kumkaribia mpaka Yahwe mwenyewwe amruhusu.