# Taarifa za jumla: Yahwe anaendelea kusema na watu wa Israeli. # Ona. "Sikiliza kwa makini." # Niko karibu kuwarudisha mateka wa Hema za Yakobo na kuwa na huruma juu ya nyumba zake. "Niko karibu kuwafanya uzao wa Yakobo kufanikiwa na nitakuwa na huruma juu yao." # Kisha mji utajengwa juu ya lundo la magofu. "Kisha wataujenga Yerusalemu juu ya magofu yake" # Kisha wimbo wa kusifu na sauti ya shangwe itasikika kutoka kwao. "Kisha wataimba wimbo wa kusifu na furaha." # Kwa maana nitawaongeza na wala sitawapunguza. Virai hivi vyote vinamaana kwamba Mungu ataisababisha idadi ya watu wa Israeli kuongezeka. # Ili kwamba wasifanywe wanyonge. "Ili kwamba asiwepo mtu wa asiwepo mtu wa kuwashusha."