# Maelezo ya jumla: Yahwe anaendelea kusema kwa watu wa Israeli. # Mtumishi wangu Yakobo, usiogope ... na usikate tamaa, Israeli. Virai vyote vina maana moja. Cha pili kinakipa nguvu cha kwanza. # Maana ona. "Sikilizeni kwa makini." # Na usikate tamaa. "Na usihuzunike." # Niko karibu kukurudisha kutoka mbali, na uzao wako kutoka nchi ya utumwa. Virai hivi via maana moja; cha pili kinakipa nguvu cha kwanza. # Kutoka nchi ya utumwa. "Kutoka sehemu ambako mlikuwa mateka." # Yakobo atarudi. "Watu watarudi kwenye nchi yao." # Ataokolewa. "Watu watakuwa salama." # Ambako nimewatawanya. "Niliko watuma." # lakini hakika sitakuacha. "Lakini sitakuharibu kabisa kabisa." # Sitakuacha bila kukuadhibu. "hakika nitakuadhibu."