# Maelezo ya jumla: Yahwe anaendelea kusema kwa Waisraeli. # Nitaivunja nira ya shingo zenu, na Nitaisambaza minyororo yenu. Maneno haya yote yanaonesha kwamba Yahwe atawaweka huru watu wake wa Israeli dhidi ya utumwa. # Watamwabudu Yahwe. Neno "wata" linataja watu wa uzao wa Yakobo. # kumtumikia Daudi mfalme wao. Hapa anatajwa mmoja wa wazawa wa Daudi.