# kiti cha Daudi Hii ina maana ya kuwa na mamlaka ya kifalme, kama vile Daudi alivyokuwa nayo. AT "kutawala kama mfalme, kama Daudi mbele yenu" # kusikiliza neno la Bwana "kuwa makini kwa neno la Bwana" # wewe na watumishi wako, na watu wako "wewe na watumishi wako, na watu wako wanaoishi katika nchi yake" # mnaokuja kwa malango haya Haya ni malango ya jumba la mfalme. AT "ambaye anakuja kumtembelea mfalme" # mkono wa mshindani Neno "mkono" linamaanisha nguvu au udhibiti wa mtu. # Usimtendee mabaya Usimtendee mtu vibaya # yatima mtoto ambaye hana wazazi # Usifanye......kumwaga damu isiyo na hatia "Usifanye ... kuwaua watu wasio na hatia" # mahali hapa "mahali hapa" linamaanisha Yerusalemu, au hata nchi nzima ya Yuda. Hii haina maana kuwa ni vizuri kuua watu katika maeneo mengine.