# mali yako yote pamoja na hazina zako zote Maneno "mali" na "hazina" yanamaanisha kitu kimoja na kutaja kitu chochote ambacho wanaona kuwa cha thamani. # nyara Hii inahusu mambo ambayo watu huiba au kuchukua kwa nguvu. # dhambi iliyo katika maeneo yako yote "umetenda kila mahali" # urithi Hii inahusu nchi ya Israeli. # umewasha moto katika ghadhabu yangu, ambao utakawaka milele Bwana anafananisha hukumu yake na moto unaoharibu. AT "kwa kunifanya niwe mwenye hasira, ni kama umeanza moto ambao utakuunguza"