# Taarifa kwa ujumla BWANA anaendelea kuongea juu ya watu wa Yuda. # binti wa watu wangu Tazama 4:11 # Ndimi zao ni mishale iliyochongoka Ndimi huumiza watu kwa uongo katika njia sawa na mishale iliyochongoka inavyoumiza # Kwa midomo yao wanatangaza amani pamoja na jirani zao "Wanasema kwa maneno yao kuwa wanataka amani na majirani zao." # lakini katika mioyo yao wanadanganya wakati wa kusubiri "lakini katika uhalisia wanataka kuwaangamiza jirani zao." # Kwa nini nisiwaadhibu kwa sababu ya mambo haya ... kwa nini nisijilipizie kisasi kwa taifa ambalo liko kama hili? Tazama 5:7