# Taarifa kwa ujumla BWANA anaendelea kuongea na Yeremia juu ya watu wa Yuda. # Kila mmoja wenu neno "wenu" linawawakilisha watu wa Yuda # awe mlinzi wa jirani yake na usimwamini hata ndugu yako yeyote "uwemwangalifu kwa kutowaamini ndugu zako Waisraeli, na usimwamini hata ndugu yako" # kila jirani anatembea akilaghai Tabia ya kuongea uongo juu ya kila mmoja ni ulagahai. # Kila mwanamuume anamkejeli jirani yake na haongei ukweli "Watu wote wanakejeliana na hawasemei ukweli" # Ndimi zao hufundisha vitu vya uongo "wanafundisha vitu ambavyo si vya ukweli." # Hujidhofisha ili kusema uongo "wamechoka kwa sababu ya kutenda maovu mengi" # makazi yenu yako kati ya udanganyifu kuishi na miongoni mwa waongo ni sawa na kuishi katikati ya uongo. # kwa uongo wao wanakataa kunitambua mimi "Kwa kusema uongo huu wote, watu wa Yuda wameshindwa kunitii mimi kama Mungu." # asema BWANA Tazama 1:7